Switzerland
Klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia anayochezea Cristiano Ronaldo imepigwa marufuku na Fifa kusajili wachezaji hadi itakapoilipa Leicester City deni lililotokana na usajili wa aliyekuwa winga wa timu hiyo, Ahmed Mussa (pichani).
Mwaka 2018, Leicester iliwauzia Al Nassr mchezaji huyo kutoka Nigeria lakini baadaye timu hizo mbili zikaingia katika mzozo wa malipo na ndipo Leicester ilipoamua kuwasilisha malalamiko yake Fifa ikidai ilipwe Dola 390,000.
“Adhabu hiyo itafutwa mara tu baada ya kulipwa kwa deni hilo na kuthibitishwa na upande wa mdai,” ilieleza kwa kifupi taarifa ya Fifa.
Klabu ya Al Nassr imejipatia umaarufu dunia katika siku za hivi karibuni baada ya kumsajili winga wa zamani wa Real Madrid na Man United, Cristiano Ronaldo.
Mbali na Ronaldo, Al Nassr pia hivi karibuni imekamilisha usajili wa nyota wa Croastia, Marcelo Brozovic huku kukiwa na habari pia ipo katika mkakati mzito wa kumsajili kwa pesa ndefu nyota wa Chelsea, Hakim Ziyech.
Klabu hiyo hata hivyo haijasema lolote kuhusu deni hilo ingawa ni ukweli kwamba mwaka 2018 ilimsajili winga huyo wa Nigeria kutoka Leicester.
Kimataifa Fifa yaifungia Al Nassr kusajili
Fifa yaifungia Al Nassr kusajili
Read also
