Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Singida Fountain Gate, Hans Pluijm (pichani) amesema ameanza mapema kusuka kikosi chake kuelekea mechi yao ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.
Singida imerejea mazoezini rasmi wiki hii ikianza maandalizi kuelekea msimu ujao lakini Pluijm amesema wanahitaji kufanya vizuri kwanza kwenye mechi za Ngao ya Jamii kabla ya msimu kuanza, hivyo wanajipanga vilivyo.
“Tumeanza maandalizi rasmi wiki hii na tayari wachezaji wetu wengi wa nje ya nchi wameanza kuwasili, tunahitaji kuwa na maandalizi mazuri zaidi kwa sababu tuna mtihani kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.
“Kila mtu anafahamu Simba ni wazuri, wanaendelea kujipanga kuelekea msimu ujao, nasi pia tunaisuka timu kwa ajili ya msimu mpya ambao tutashiriki michuano mingi, ni lazima tuwe na kipimo cha ubora wa sawasawa na kuanza lazima tujipange kufanya vizuri dhidi yao,” alisema Pluijm.
Singida ambayo msimu ujao kwa mara ya kwanza itashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, itaumana na Simba katika mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii Agosti 10, mwaka huu. Nusu fainali nyingine ni Yanga dhidi ya Azam, mechi zote zikipigwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Soka Pluijm ajiandaa kuikabili Simba
Pluijm ajiandaa kuikabili Simba
Read also
