Na mwandishi wetu
Mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ ameeleza kukaribia kukata tamaa ya kuwekeza katika klabu hiyo kutokana na kuchelewa kukamilika kwa mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji.
Dewji ameyaeleza hayo leo Jumanne katika andiko aliloliweka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter akibainisha kuwa ni miaka sita sasa mchakato huo unaendelea na haumaliziki.
“Transformation (mabadiliko) ya Simba bado haijakamilika, huu ni mwaka wa sita, karibuni nitakata tamaa,” aliandika Dewji ambaye pia ni rais wa heshima wa klabu hiyo.
Simba ilianza mchakato huo tangu mwaka 2018 ikiwa ni mahsusi kwa ajili ya kuitoa timu hiyo kwenye mfumo wa wanachama na kwenda kwenye kampuni lakini hadi sasa mabadiliko hayo hayajakamilika.
Wekundu hao waliamua kufanya hivyo baada ya kubaini kuwa mfumo wa wanachama hautawapa mafanikio na maendeleo kulingana na mifumo ya soka na kiuendeshaji kidunia kwa sasa ilivyo.
Katika mabadiliko hayo, Dewji anawekeza kiasi cha Shilingi bilioni 20 ambazo ambazo ni sawa na umiliki wa hisa asilimia 49 na mmiliki mwenza ambaye ni wanachama wakimiliki asilimia 51.
Pamoja na hayo, hatua za awali za kubadilishwa kwa mfumo zilishaanza kuchukuliwa ikiwemo mabadiliko ya muundo wa uongozi wa klabu hiyo kwa kuundwa bodi ya wakurugenzi, uwepo wa mtendaji mkuu na mengineyo huku mchakato kamili ukiwa bado haujakamilika.
GreenSports ilifanya juhudi za kumtafuta Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula kutoa ufaftisanuzi walipofikia katika mabadiliko hayo lakini simu yake ya mkononi iliita bila ya kupokelewa, alipotafutwa meneja mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally simu yake ya mkononi haikuwa hewani.
Soka Mo Dewji atishia kukata tamaa
Mo Dewji atishia kukata tamaa
Read also
