Na mwandishi wetu
Baada ya kukamilisha usajili wa kujiunga na JKT Tanzania, kiungo wa zamani wa Simba, Hassan Dilunga amesema kuwa Simba haina baya kwake na anaitakia kila la heri kuelekea msimu ujao wa 2023/24.
Dilunga (pichani) ambaye alicheza Simba kwa misimu mitatu, ameingia mkataba wa miaka miwili ikiwa ni wiki chache tangu aonekane akifanya mazoezi na Simba baada ya kuuguza jeraha la goti kwa msimu mzima.
Awali ilielezwa kuwa kiungo huyo anakaribia kusaini mkataba mpya na Wekundu hao lakini juzi akaonekana ametua JKT na kuibua sintofahamu.
“Niliongea vitu kadhaa na kocha Roberto Oliveira (kocha wa Simba), nikazungumza na uongozi tukakubaliana, sina vingi sana vya kuvielezea badala yake ninachojua kutoka kwenye sakafu ya moyo wangu, Simba hawana baya kwangu.
“Wamenisaidia sana kipindi cha matibabu hadi napona, wanaonijua Dilunga wanatambua ukweli ni upi nimekaa chini na familia yangu nikaona acha iwe zamu ya JKT Tanzania,” alisema Dilunga.
Alisema ni kweli kuna raha yake kuichezea Simba, lakini wakati mwingine mengine yanabaki ya ndani na anawatakia Simba msimu mzuri kwani anajua aliifanyia kila kitu na ilimthamini hivyo ni wakati wa kutafuta changamoto nyingine.
Soka Dilunga aaga Simba, atua JKT
Dilunga aaga Simba, atua JKT
Read also
