Na mwandishi wetu
Azam FC imetangaza kumnasa kiungo mshambuliaji wa Raja Casablanca ya Morocco, Djibril Sillah (pichani) anayetarajiwa kutua nchini hivi karibuni.
Azam imeeleza hayo leo Jumatano kupitia majukwaa yake mtandaoni ikifafanua kuwa nyota huyo raia wa Gambia atatua nchini muda wowote kuanzia sasa kukamilisha taratibu za usajili huo.
Sillah anayetajwa kufunga mabao saba na kutoa pasi za mabao manne kwenye Ligi Kuu ya Morocco msimu uliopita alipokuwa akiitumikia JS Soualem kwa mkopo, anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Azam FC kuelekea msimu ujao baada ya Feisal Salum ‘Fei Toto’.
Mchezaji huyo, 24 aliyewahi kuwika na kikosi cha Fortune FC ya kwao mbali na kumudu majukumu ya kiungo wa kati pia anamudu nafasi za kiungo mshambuliaji wa pembeni.
Soka Kiungo wa Raja atua Azam
Kiungo wa Raja atua Azam
Read also