Na mwandishi wetu
Klabu ya Singida Fountain Gate, imeendelea kujiweka sawa kwa ajili ya msimu ujao ikiwa tayari imewaongezea mikataba wachezaji wake watatu kwa pamoja; viungo Yusuf Kagoma, Aziz Andabwile na kipa Benedict Haule.
Timu hiyo imeeleza hayo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, ikifafanua kuwa imewaongezea wachezaji hao mikataba itakayofikia tamati mpaka mwaka 2026.
Wachezaji hao wameongezewa mikataba baada ya kazi nzuri waliyoonesha wakiwa na timu hiyo tangu walipotua msimu wa 2022-23 na kuisaidia kumaliza nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu NBC na kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.
Kocha wa Singida, Hans Pluijm akizungumza na GreenSports leo Jumanne, aliwataja wachezaji hao kuwa ni miongoni mwa wachezaji muhimu katika kikosi chao, hivyo ni maamuzi sahihi kwa faida ya kikosi kizima kulingana na michuano waliyonayo msimu ujao.
Mbali na hao watatu, siku chache zilizopita Singida pia iliweka wazi kumuongeza mkataba kiungo wake Mbrazil, Bruno Gomes atakayekuwa na timu hiyo mpaka mwaka 2025.
Soka Watatu waongezewa mikataba Singida FG
Watatu waongezewa mikataba Singida FG
Related posts
Read also
