Na mwandishi wetu
Rais wa heshima wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ amemshukuru na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya biashara nchini Tanzania yaliyompelekea kushinda tuzo ya All Africa Business Leaders Awards 2023 upande wa viwanda.
Dewji ameshinda tuzo hiyo kwenye kipengele cha Industrialist of the Year usiku wa kuamkia leo Jumamosi katika hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Sun City, Johannesburg, Afrika Kusini.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, mwekezaji huyo wa Simba SC alieleza furaha yake ya kushinda tuzo hiyo na kumshukuru Rais Samia kwa matunda hayo baada ya kuwarahisishia mazingira ya biashara nchini.
“Nimeheshimiwa na napokea kwa unyenyekevu Tuzo ya All Africa Business Leaders kwa Industrialist of the Year 2023. Naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa Rais wa Tanzania, mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kujenga mazingira mazuri ya biashara nchini ambayo yanawezesha maendeleo makubwa ya viwanda nchi nzima,” aliandika Dewji.
Mbali na tuzo hiyo, Februari, mwaka huu pia jarida la Forbes lilimuorodhesha Dewji kuwa tajiri namba 13 Afrika akifungana na wengine wawili katika nafasi hiyo kwa utajiri wa Dola za Marekani bilioni 1.5 (sawa na Sh 3.5 trilioni).
Kimataifa Mo Dewji amshukuru Rais Samia
Mo Dewji amshukuru Rais Samia
Read also
