London, England
Arsenal imekubali kutoa kitita cha Pauni 65 milioni kumsajili mshambuliaji wa Chelsea, Kai Havert (pichani) ambaye amekuwa katika hesabu za kocha Mikel Arteta kwa muda mrefu sasa.
Arteta amepania kuimarisha kikosi chake ambacho kimeshindwa kubeba taji la Ligi Kuu England (EPL) msimu wa 2022-23 baada ya kuvurunda katika mechi chache za mwisho na hatimaye taji hilo kubebwa na Man City.
Inadaiwa klabu hizo mbili zimefanya makubaliano ya awali na ya msingi ingawa mchezaji bado atakuwa na fursa ya kujadiliana na Arsenal kuhusu maslahi binafsi na hatimaye kufanyiwa vipimo vya afya.
Kwa mantiki hiyo huenda gharama za uhamisho za Havert zikaongezeka lakini haijajulikana iwapo nyongeza hiyo kwa ujumla itafikia Pauni 71 milioni ambazo Chelsea ilizitumia mwaka 2020 kumsajili mchezaji huyo kutoka Bayer Leverkusen ya Ujeumani.
Mwaka 2021, Havert aliifungia Chelsea bao katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Man City na kuiwezesha timu hiyo kubeba taji hilo.
Baada ya kukamilisha usajili wa Havert, Arsenal sasa inaendelea kupigania usajili wa nahodha na kiungo wa West Ham na timu ya Taifa ya England, Declan Rice ingawa majuzi West Ham ilikataa kwa mara ya pili ofa ya Arsenal ya Pauni 90 milioni.
Kimataifa Arsenal yamnasa Kai Havertz
Arsenal yamnasa Kai Havertz
Read also
