Manchester, England
Klabua Manchester United inaamini kwamba ipo katika hatua za mwisho za kukubaliana na mshambuliaji wake, Marcus Rashford ili asaini mkataba mpya wa muda mrefu.
Rashford anaelekea kufikia mwisho wa mkataba wake na klabu hiyo katika kipindi hiki cha kiangazi na baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kuahirishwa mwaka jana, mchezaji huyo anadaiwa kuwa mbioni kusaini mkataba huo hivi karibuni.
Habari za ndani zinadai kwamba klabu hiyo inajiandaa kumuongezea marupurupu mshambuliaji huyo kutokana na mchango wake mkubwa kwenye timu hiyo msimu uliopita na huenda akawa mmoja wa wachezaji wanaolipwa pesa ndefu katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Rashford mwenye umri wa miaka 25 amekuwa kivutio katika msimu wake wa kwanza Man United chini ya kocha mpya Erik ten Hag akifunga mabao 30 katika mashindano yote, 17 kati ya hayo akiyafunga kwenye Ligi Kuu England.
Mafanikio ya mshambuliaji huyo chini ya Ten Hag yamekuwa sababu kubwa ya mchezaji huyo kuwa tayari kuchukua uamuzi wa kuendelea kuichezea timu hiyo kwa msimu ujao wa 2023-24.
Wakati yote hayo yakiendelea vigogo wa Ufaransa, PSG nao wamekuwa wakimuwinda mshambuliaji huyo kwa muda mrefu huku pia kukiwa na habari kwamba kocha mpya wa Chelsea, Mauricio Pochettino naye anavutiwa na soka la mchezaji huyo na angependa kuona akiichezea Chelse msimu ujao.
Kimataifa Man United haina wasiwasi na Rashford
Man United haina wasiwasi na Rashford
Read also
