Manchester, England
Klabu ya Manchester United imeamua kuachana na mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Hotspur na timu ya Taifa ya England, Harry Kane.
Kane ambaye kwa muda mrefu amekuwa na mafanikio na Spurs alikuwa akiwindwa na vijogoo hao wa jiji la Manchester kabla ya taarifa iliyopatikana leo na gazeti moja la Uingereza ikidai kwamba klabu hiyo imejiondoa katika mbio hizo.
Kane ambaye imewahi kudaiwa kwamba anataka changamoto mpya nje ya Spurs, mbali ya kutakiwa na Man United pia alikuwa akiwindwa na klabu za Real Madrid ya Hispania na Bayern Munich ya Ujerumani.
Wakati Bayern ikionekana kuwa kimya katika mbio hizo, hali ni tofauti kwa Real Madrid ambayo pia imekuwa ikisaka mshambuliaji mpya baada ya kuondoka kwa Karim Benzema aliyejiunga na klabu ya Al-Ittihad ya Saudi Arabia.
Real Madrid hata hivyo inadaiwa pia kumuwinda mshambuliaji wa PSG ya Ufaransa, Kylian Mbappe ambaye zipo habari kwamba klabu yake inataka kumuuza baada ya mchezaji huyo kusema kwamba hatoongeza mkataba.
Mkataba wa Mbappe na PSG unafikia ukomo mwaka 2024 na klabu hiyo inataka kumuuza ili kuepuka kumuona akiondoka bila kupata chochote mara baada ya msimu ujao kwani atakuwa mchezaji huru.
Kimataifa Man United haimtaki tena Kane
Man United haimtaki tena Kane
Read also
