Na mwandishi wetu
Mabao saba aliyofunga Saido Ntibazonkiza wa Simba katika mechi mbili za mwisho za Ligi Kuu NBC msimu huu yamemfanya afungane mabao ya kufunga na Fiston Mayele kila mmoja akiwa na mabao 17.
Kwa kipindi kirefu Mayele amekuwa kinara wa mabao wa ligi hiyo akiwa na mabao 16 wakati Ntibazonkiza alikuwa na mabao 10 kabla mambo hayajabadilika katika mechi mbili za mwisho.
Katika mechi hizo, Ntibazonkiza alifunga mabao matano peke yake dhidi ya Polisi Tanzania katika ushindi wa 6-1 na leo Ijumaa amefunga mabao mawili katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Coastal Union.
Kwa matokeo ya mechi hizo za mwisho za ligi msimu wa 2022-23, wachezaji hao wanakuwa wamefungana kwa idadi ya mabao ya kufunga ingawa Ntibazonkiza anajivunia kwa kuwa na asisti nyingi, 12 dhidi ya nne za Mayele.
Katika vita ya kujinasua na janga la kucheza play-offs, mambo hayakuwa mazuri kwa timu za Mbeya City na KMC ambazo zitalazimika kucheza mechi hizo. KMC imeshika nafasi ya 13 licha ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mbeya City.
Ushindi wa KMC umeifanya timu hiyo ifikishe pointi 32 ambazo hazikuweza kuitoa katika nafasi ya 13 wakati Mbeya City iliyokuwa nafasi ya 13 inashuka hadi nafasi ya 14 na pointi zake 31.
Polisi Tanzania inabaki nafasi ya 15 na Ruvu Shoting inabaki ikiburuza mkia katika nafasi ya 16.
Matokeo ya mechi za mwisho Ligi Kuu NBC msimu wa 2022-23 zilizochezwa leo Ijumaa ni kama ifuatavyo…
Azam 8-0 Polisi Tanzania
Coastal 1-3 Simba
Mtibwa Sugar 3-1 Geita Gold
Prisons 0-2 Yanga
Ihefu 2-0 Kagera Sugar
Mbeya City 0-1 KMC
Ruvu Shooting 0-1 Dodoma Jiji
Namungo 1-1 Singida Big
Soka Ntibazonkiza amnasa Mayele kwa mabao
Ntibazonkiza amnasa Mayele kwa mabao
Read also