Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Singida Bisg Stars, Hans Pluijm amewashukuru wachezaji wake kwa kiwango walichoonesha msimu mzima hadi yeye kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Tuzo ya Kocha Bora wa Ligi Kuu NBC 2022-23.
Pluijm raia wa Uholanzi anawania tuzo hiyo dhidi ya Nasreddine Nabi wa Yanga na Robert Oliveira ‘Robertinho’ wa Simba. Hafla ya utoaji tuzo hizo inatarajiwa kufanyika Juni 12, mwaka huu mkoani Tanga.
Kocha huyo pia alisema kwamba anashukuru kamati ya waandaaji wa tuzo hizo za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kufahamu mchango wake katika ligi msimu huu na kuthamini mchango wake katika soka.
“Hii inamaanisha kwamba watu wanaiona kazi yangu, watu wanaiona timu yetu ambayo kwa kiasi kikubwa wachezaji wangu kwa kitu walichokionesha uwanjani ndicho kimesababisha niwepo hapa, nashukuru kwa hilo kwa kweli,” alisema Pluijm.
Pluijm ameiongoza Singida BS iliyopanda kushiriki Ligi Kuu NBC msimu huu kufika nusu fainali ya Kombe la FA (ASFC) kabla ya kufungwa na Yanga bao 1-0. Pia Singida ni miongoni mwa timu ziatakazoiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya klabu Afrika msimu ujao.
Soka Pluijm ashukuru wachezaji Singida Big
Pluijm ashukuru wachezaji Singida Big
Read also
