Na mwandishi wetu
Simba imeeleza kuwa suala la usajili wa kipa mpya wa timu hiyo kuelekea msimu ujao litategemea na ripoti ya madaktari itakayoonesha kipa wao majeruhi, Aishi Manula atakaa nje kwa muda gani.
Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amefafanua kuwa upasuaji wa Manula utakaofanyika wiki hii mjini Johannesburg, Afrika Kusini ndio utakaotoa mwelekeo wa uamuzi wa kusajili kipa mpya au la.
“Kwa kuwa Manula atafanyiwa matibabu ndani ya wiki hii maana yake ni kwamba ripoti yake ya kukaa nje itafahamika wiki hii, kwa hiyo ikitoka ripoti kwamba atakaa nje muda mrefu basi hatuna budi kuingia sokoni kutafuta makipa wengine wakati huo tukimsubiri Aishi aendelee kupona,” aisema Ally.
Manula (pichani juu) ametua juzi nchini Afrika Kusini kwa ajili ya upasuaji wa nyama za paja, jeraha alilolipata Aprili 7, mwaka huu kwenye mechi ya robo fainali ya Kombe la FA (ASFC) iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Tangu hapo Simba imekuwa ikimtumia kipa namba tatu, Ally Salim huku fununu zikieleza kuwa kipa namba mbili wa Wekundu hao, Beno Kakolanya anatarajia kutimkia Singida Big Stars msimu ujao.
Na Simba ambayo inatarajia kucheza michuano ya Super League itakayoanza Agosti, mwaka huu imekuwa ikitajwa kumuwania kipa Alfred Mudekereza anayeidakia Vipers ya Uganda alikotokea kocha wa Simba wa sasa, Robert Oliveira ‘Robertinho’.
Soka Manula ashikilia hatma ya kipa mpya Simba
Manula ashikilia hatma ya kipa mpya Simba
Read also
