Madrid, Hispania
Klabu ya Real Madrid ya Hispania inatarajia kutangaza usajili wa kiungo wa Borrusia Dortmund na timu ya Taifa ya England, Jude Bellingham wakati wowote wiki ijayo.
Bellingham mwenye umri wa miaka 19 amekuwa akiwindwa na vigogo hao wa Hispania tangu baada ya fainali za Kombe la Dunia, Desemba mwaka jana na sasa inadaiwa mazungumzo yamekwenda vizuri.
Hatua hiyo itakuwa pigo kwa Man City ambayo pia ilitajwa katika mbio za kuitaka saini ya kiungo huyo kwa matumaini kwamba ingemuunganisha na Erling Haaland ambaye amewahi kuwa pamoja na Bellingham katika klabu ya Dortmund.
Haaland, mshambuliaji kinara wa mabao Man City kabla ya kujiunga na timu hiyo alikuwa akiichezea Dortmund na habari iliyokuwapo kwa muda mrefu ni kwamba naye amekuwa akiwindwa kwa muda mrefu na Real Madrid.
Kwa hali hiyo haitokuwa ajabu kwa walichokifikiria Man City kumuunganisha Haaland na Bellingham katika jiji la Manchester kikafanywa na Real Madrid kwa kuwaunganisha wachezaji hao katika jiji la Madrid.
Kimataifa Real Madrid kumtangaza Bellingham wiki ijayo
Real Madrid kumtangaza Bellingham wiki ijayo
Read also
