London, England
Beki wa pembeni, Mtanzania Novatus Dismas anayekipiga katika klabu ya Zulte Waregem ya Ubelgiji anawaniwa na timu za Southampton na Middlesbrough za England.
Novatus (pichani juu) ametajwa kuwaniwa na timu hizo kutokana na uwezo anaoendelea kuuonesha tangu ajiunge na Zulte mwanzoni mwa msimu huu akitokea Maccabi Tel Aviv ya Israel.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail la Uingereza, Southampton inayoshiriki Ligi Kuu England (EPL) inamuwania mchezaji huyo ikichuana na Middlesbrough.
Middlesbrough kwa sasa inapambana katika Ligi ya Championship wakati mambo si mazuri kwa Southampton ambayo tayari imeshuka daraja na inasubiri kucheza Championship msimu ujao.
Novatus mwenye umri wa miaka 20 ambaye ni kiungo mkabaji, akicheza kwa ufasaha pia kama beki wa pembeni, beki wa kati na kiungo wa kushoto, imeelezwa kuwa uwezo wake huo pia umezivutia timu hizo.
Licha ya timu yake kushuka daraja lakini bado Dismas ameendelea kuzivutia klabu kubwa kutokana na kiwango anachokionesha hata anapokuwa kwenye majukumua ya timu ya taifa, Taifa Stars.
Kimataifa Novatus Dismas atakiwa Southampton
Novatus Dismas atakiwa Southampton
Read also
