London, England
Beki wa zamani wa Man United na timu ya England, Rio Ferdinand, Septemba 1997, alikutwa na hatia ya kuendesha gari akiwa amelewa baada ya kukesha katika klabu ya usiku akinywa pombe.
Kwa kosa hilo, Ferdinand ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka, alipigwa marufuku kuendesha gari kwa mwaka mmoja.
Kocha wa wakati huo wa timu ya Taifa ya England, Glenn Hoddle akamuadhibu kwa kumuondoa katika kikosi chake kilichokuwa kikijiandaa kuumana na Moldova katika mechi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia 1998, mechi iliyopigwa Septemba 10, 1997.
Kwa adhabu hiyo, Ferdinand akashindwa kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa umri mdogo kuichezea timu ya Taifa ya England baada ya Duncan Edwards, Ferdinand wakati huo alikuwa na miaka 18 na miezi 10.
Ferdinand ambaye pia amewahi kuichezea Leeds United, hata hivyo aliendelea kuandamwa na matatizo ya udereva huku ulevi ukidhaniwa kuwa chanzo na kujikuta akiadhibiwa mara kadhaa ikiwamo kutozwa faini na wakati mwingine kufungiwa kuendesha gari.
Machi 2003 alifungiwa kuendesha gari kwa miezi sita pamoja na kutozwa faini ya Pauni 2,500 baada ya kukamatwa na askari wa usalama barabarani akiwa anaendesha gari kwa mwendo wa kasi (km 148/h).
Miaka miwili baadaye alikutwa na kosa hilo hilo na kutozwa faini ya Pauni 1,500 safari hii mahakama ilimtaka ajirekebishe na kuwa mfano wa kuigwa katika jamii badala ya kufanya kosa lile lile zaidi ya mara moja wakati anatakiwa kuwa mwanamichezo mfano wa kuigwa katika jamii hasa kwa vijana.
Agosti 2020, kwa mara nyingine Ferdinand alirudia kosa lile lile, safari hii alitakiwa kulipa faini ya Pauni 822 pamoja na gharama nyingine.
Kimataifa Pombe ilipomnyima rekodi Rio Ferdinand
Pombe ilipomnyima rekodi Rio Ferdinand
Read also
