London, England
Klabu ya Tottenhham Hotspur imeanza mazungumzo kwa mara nyingine na kocha wa zamani wa Bayern Munich, Julian Nagelsmann ili ainoe timu hiyo ambayo hivi karibuni iliachana na Antonio Conte.
Nagelsmann (pichani) hata hivyo ametaka kabla ya kukubali kibarua hicho ajue nani atakuwa mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo ambayo kwa sasa mambo yake si mazuri kwenye Ligi Kuu England (EPL).
Hii si mara ya kwanza kwa Spurs kuhusishwa na kocha huyo ingawa kinachoonekana sasa ni kwamba klabu hiyo imeongeza nguvu katika mpango huo na matumaini ya kumpata kocha huyo ni makubwa.
Mambo si mazuri kwa Spurs kwani imetoka katika mbio za kuwania nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao ikiiacha vita hiyo kwa klabu za Man United, Newcastle na Liverpool.
Timu hiyo pia huenda ikakimbiwa na mshambuliaji wake mahiri, Harry Kane ambaye amekuwa akihusishwa na mipango ya kujiunga na klabu kadhaa ikiwamo Man United na PSG ya Ufaransa.
Na ingawa Kane hajaamua atakapoelekea kitendo cha Spurs kutoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao ni sababu tosha kwa mshambuliaji huyo ambaye pia ni nahodha wa timu ya England aondoke.
Kimataifa Spurs yamrudia Nagelsmann
Spurs yamrudia Nagelsmann
Read also
