Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele amesema anapambana kuhakikisha Yanga inatwaa Kombe la Shirikisho Afrika kisha masuala ya ufungaji bora yatakuwa baadaye maana hilo ni la kwake binafsi.
Mayele hadi sasa anaongoza kwenye michuano hiyo akiwa na mabao sita sawa na Ranga Chivaviro wa Marumo Gallants lakini wakifuatiwa kwa karibu na Khaled Bousseliou wa USM Alger ya Algeria mwenye mabao manne.
Alisema anafahamu Khaled anaweza kumpiku kwenye mechi mbili za fainali watakazokutana lakini haangalii hilo, kwa sasa anatazama namna ya kuisaidia Yanga kuandika historia ya kutwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza.
“Mimi nataka kuipambania timu yangu, tufanikiwe kuchukua kombe, hivyo vingine baadaye kwanza timu sababu tunataka kuandika historia kwa timu yetu na Tanzania. Tuna mechi mbili za fainali, tutahakikisha tunatumia nafasi vizuri,” alisema Mayele.
Kuhusu wapinzani wao, USMA, Mayele alisema anaiheshimu kwani mpaka imefika fainali ni timu nzuri hivyo watahakikisha wanapata matokeo kwenye mechi ya nyumbani kabla ya kwenda ugenini.
Mechi ya kwanza inatarajiwa kupigwa Mei 28 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kabla ya mechi ya marudiano itakayopigwa Juni 3.
Kimataifa Mayele: Kombe kwanza ufungaji bora baadaye
Mayele: Kombe kwanza ufungaji bora baadaye
Read also