London, England
Klabu za Newcastle na Man United zimeingia vitani kila moja ikiwania kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich, Sadio Mane (pichani) ambaye mambo yake si mazuri katika klabu hiyo.
Mane mwenye umri wa miaka 31, msimu uliopita alitamba na Liverpool na ndiye aliyeiwezesha timu ya Senegal kutwaa taji la Mataifa ya Afrika, tangu atue Bayern msimu huu amekuwa na wakati mgumu.
Kasi yake ya upachikaji mabao iliyozoeleka inaonekana kupotea huku akiandamwa na majanga ya hapa na pale ikiwamo tukio la hivi karibuni la kumpiga ngumi mchezaji mwenzake, Leroy Sane.
Baada ya tukio hilo lililotokea kwenye mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Man City na Bayern kulala kwa mabao 3-0, Bayern ilimsimamisha Mane na akakosa mechi moja.
Baada ya tukio hilo habari mpya zilianza kuibuka kwamba Bayern inajiandaa kumpiga bei na sasa Man United na Newcastle zimeonekana kuwa mstari wa mbele kila moja ikiitaka saini ya mchezaji huyo.
Man United na Newcastle zote zipo vizuri kwenye Ligi Kuu England (EPL) katika kupigania nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao hivyo kama kigezo cha Mane kitakuwa na michuano hiyo, atakuwa huru kuchagua mojawapo ya timu hizo.
Katika EPL, Newcastle inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 69 katika mechi 36 wakati Man United inashika nafasi ya nne baada ya kucheza mechi 35.
Kimataifa Sadio Mane aziingiza vitani Man Utd, Newcastle
Sadio Mane aziingiza vitani Man Utd, Newcastle
Read also
