Barcelona, Hispania
Barcelona hatimaye imetwaa taji la La Liga msimu wa 2022/23 kwa kishindo baada ya kuichapa Espanyol mabao 4-2 ikilitwaa taji hilo mara ya pili baada ya kufanya hivyo msimu wa 2018-19.
Barca imelibeba taji ikiwa na mechi nne mkononi, ina pointi 85 imewazidi mahasimu wao Real Madrid wanaoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi 14 ambazo hawawezi kuzifikia kwa mechi zilizobaki.
Vinara hao waliutawala vyema mchezo kuanzia kipindi cha kwanza na kupata bao la kwanza dakika ya 11 lililofungwa na Roberto Lewandowski kabla Balde hajaongeza la pili dakika ya 20.
Lewandowski ambaye amekuwa na ukame wa mabao, aliongeza bao la tatu dakika ya 40 ambalo ni bao lake la 20 na kuzifanya timu hizo ziende mapumziko Barca ikiwa mbele kwa mabao 3-0.
Dakika nane baada ya kuanza kipindi cha pili, Barca iliandika bao la nne lililofungwa kwa kichwa na Jules Kounde lakini Espanyol walipambana na kupata mabao mawili ya kufutia machozi yaliyofungwa na Javier Puado dakika ya 73 na Joselu katika dakika mbili za nyongeza.
Taji hilo linakuwa la kwanza kwa kocha Xavi ambaye wakati akiichezea Barca anajivunia rekodi ya kubeba taji la La Liga mara nane katika miaka 17 aliyotamba na timu hiyo.
Kwa nahodha Sergio Busquets taji hilo ambalo ni la tisa kwake limempa jambo la kujivunia wakati akiiaga timu hiyo, akihitimisha miaka yake 18 ya mafanikio ndani ya klabu hiyo kwani tayari ametangaza kustaafu baada ya msimu huu.
Kwa upande mwingine Barca kwa sasa inajiandaa kuufanyia marekebisho uwanja wake wa Nou Campo ingawa mashabiki watapata nafasi ya kulifurahia taji hilo kwenye uwanja huo kwenye mechi mbili zilizobaki dhidi ya Real Sociedad na Real Mallorca.
Maatokeo mechi nyingine za La Liga
Espanyol 2-4 Barcelona
Celta Vigo 1-2 Valencia
Elche 1-0 Atl Madrid
Real Valladolid 0-3 Sevilla
Kimataifa Barca yatwaa taji La Liga
Barca yatwaa taji La Liga
Read also