London, England
Klabu ya Southampton leo Jumamosi imehitimisha miaka yake 11 kwenye Ligi Kuu England (EPL) kwa kushuka daraja baada ya kukubali kipigo cha nyumbani cha mabao 2-0 mbele ya Fulham.
Fulham walipata bao lao la kwanza dakika ya 48 lililofungwa na Carlos Vinicius kabla ya Alksandar Mitrovic hajamalizia bao la pili dakika ya 72 na kuhitimisha safari ya Southampton katika EPL.
Kwa Mitrovic bao hilo ni la 12 msimu huu na linakuwa na maana kubwa kwani hiyo ndio mechi yake ya kwanza baada ya kufungiwa mechi nane kwa kosa la kumsukuma mwamuzi Chris Kavanagh.
Mechi hiyo ilikuwa muhimu kwa Southampton kushinda ili walau kufufua matumaini ya kuendelea kucheza EPL msimu ujao lakini kwa hali ilivyo hata wakishinda mechi mbili zilizobakia watafikisha pointi 30 ambazo haziwezi kuwasaidia wasiwe moja ya timu zinazoshuka daraja.
Kwa maana hiyo, Southampton msimu ujao wa 2023-24 itaanza rasmi kushiriki ligi ya Championship ambayo mara ya mwisho ilishiriki mwaka 2012.
Matokeo ya mechi za EPL zilizochezwa leo Jumamosi ni kama ifuatavyo…
Leeds 2-2 Newcastle
Aston Villa 2-1 Tottenham
Chelsea 2-2 Nottm Forest
Crystal Palace 2-0 Bournemouth
Man Utd 2-0 Wolves
Southampton 0-2 Fulham
Kimataifa Southampton yashuka daraja
Southampton yashuka daraja
Read also
