Na mwandishi wetu
Kipa namba tatu wa Simba, Ally Salim amewashukuru wachezaji wenzake pamoja na mashabiki kwa kumuwezesha kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Aprili
Alisema kuwa hilo ni jambo la furaha kwake kushinda tuzo hiyo na kuweka rekodi ya kuwa mlinda mlango wa kwanza kushinda tuzo hiyo iliyoanzishwa miaka miwili iliyopita na kwamba itamuimarisha zaidi.
“Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu, nawashukuru wachezaji wenzangu pamoja na mashabiki kwa kunipigia kura mpaka kushinda tuzo hii, ina maana kubwa kwangu, naamini itaniimarisha zaidi,”alisema Ally.
Ofisa Uhusiano wa Emirate Aluminium wanaodhamini tuzo hiyo, Issa Maeda amempongeza Ally kwa kuonyesha kiwango bora mwezi Aprili na kuisaidia timu kupata matokeo mazuri.
“Katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Ihefu ukaja dhidi ya Yanga na hata ule wa nyumbani na Wydad Casablanca alionyesha kiwango bora na tunampongeza kwa hilo.”
“Mara kadhaa Aishi Manula amewahi kuingia fainali ya kinyang’anyiro hiki lakini alizidiwa na wachezaji wa ndani ila Ally Salim ameweza na kuweka historia,” alisema Maeda.
Ally amekabidhiwa pesa taslimu Sh 2,000,000 (milioni mbili) na tuzo kutoka kwa wadhamini hao baada ya kuwashinda Jean Baleke na Kibu Denis alioingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.
Soka Ally Salim awashukuru mashabiki
Ally Salim awashukuru mashabiki
Read also
