London, England
Arsenal jana Jumanne iliichapa Chelsea mabao 3-1 na kushika usukani wa Ligi Kuu England (EPL) ingawa huenda furaha yao ikafikia ukomo leo Jumatano usiku.
Kwa ushindi huo Arsenal inaongoza ligi ikiwa na pointi 78 ikifuatiwa na Man City yenye pointi 76 ingawa City imecheza mechi 32 na Arsenal 34 na leo City inaumana na West Ham.
Ushindi wowote leo utaifanya City iiengue Arsenal kileleni na hivyo kuifanya timu hiyo iliyoshika usukani kwa muda mrefu kurejea katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Rekodi nzuri ya Arsenal ilianza kuharibika hivi karibuni baada ya kucheza mechi nne bila ushindi na hapo hapo ikaambulia kichapo mbele ya Man City ambao Jumapili waliwaengua Arsenal kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya ushindi walioupata kwa Fulham.
Mabao ya washindi katika mechi hiyo yalifungwa na Odegaard aliyefunga mawili na Gabriel Jesus aliyefunga bao moja wakati bao pekee la Chelsea lilifungwa na Madueke.
Kwa upande mwingine mambo yameendelea kuwa mabaya kwa Chelsea na kocha wao wa muda, Frank Lampard ambaye anaishuhudia timu hiyo ikipata kipigo cha sita mfululizo na hivyo kuzidisha habari kwamba kocha huyo hana nafasi au nafasi yake ndogo mno Chelsea.
Kimataifa Arsenal yarejea kileleni lakini…
Arsenal yarejea kileleni lakini…
Read also