Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele ametajwa kuwa mfungaji wa bao bora la wiki katika mechi za mkondo wa kwanza hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Mayele ameibuka kidedea kupitia bao la kwanza alilofunga kwa kumchambua kipa baada ya kupokea pasi ya Bakari Mwamnyeto katika ushindi wa ugenini wa mabao 2-0 dhidi ya Rivers United ya Nigeria.
Mshambuliaji huyo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo alifunga mabao yote mawili katika mechi hiyo na kuwa kinara wa mabao akifikisha matano huku akiwa amefungana na Ranga Chivavilo wa Marumo Gallants ya Afrika Kusini.
Katika wiki ya mechi hizo, Mayele pia aliiongoza Yanga kuwa timu pekee iliyoibuka na ushindi wa ugenini katika mechi nne za robo fainali za michuano hiyo.
Upande wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambako Tanzania inawakilishwa na Simba, mfungaji wa bao bora la wiki la michuano hiyo ni Mohamed Abdelmonem wa Al Ahly walipoinyoosha Raja Casablanca mabao 2-0.
Shirikisho la Soka Afrika (Caf) waliotaja washindi hao pia taarifa yao ilieleza kuwa Mohamed anayemudu majukumu ya beki wa kati kuwa ni mchezaji bora wa wiki wa Ligi ya Mabingwa, akiwemo pia kwenye kikosi bora cha wiki cha michuano hiyo.
Kimataifa Mayele afunga bao bora Afrika
Mayele afunga bao bora Afrika
Read also
