Manchester, England
Man City imeichapa Bayern Munich mabao 3-0 huku Erling Haaland akifunga bao moja kati ya hayo na kufikisha mabao 45 katika mechi 39 za msimu huu na kuweka rekodi ya kipekee kwa mchezaji wa Ligi Kuu England (EPL).
Mshambuliaji wa zamani wa Man United, Ruud van Nistelrooy aliifungia timu hiyo mabao 44 katika msimu wa 2002-03 na Mohamed Salah naye alifikisha mabao kama ya Van Nistelrooy katika msimu wa 2017-18.
Haaland sasa anakuwa amevunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na mastraika hao, tofauti ya Van Nistelrooy na Salah ni kwamba wao walitumia mechi 52 kila mmoja kufikisha rekodi ya mabao 44 ikiwa ni tofauti ya mechi 13 za Haaland ambaye tayari amefikisha mabao 45 na kuwazidi wote wawili.
Haaland ambaye ni nyota wa zamani wa Borussia Dortmand sasa anakuwa amewafunga Bayern mara sita tangu atue Man City ingawa alikutana na timu hiyo mara kadhaa katika Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga kabla ya kutua Man City.
Mshambuliaji wa zamani wa Bayern na timu ya Taifa ya Ujerumani, Mario Gomez, akimzungumzia Haaland alisema kwamba kwa mambo anayoyafanya kila timu inalazimika kumhofia.
Kwa ushindi huo ambao ni wa mechi ya kwanza ya robo fainali, Man City sasa inasubiri kurudiana na timu hiyo mjini Munich, katika mechi ambayo ushindi au sare yoyote vitaifanya timu hiyo ifuzu hatua ya nusu fainali.
Katika mechi nyingine ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyochezwa jana Jumanne, Benfica ikiwa nyumbani ililala kwa mabao 2-0 mbele ya Inter Milan.
Mechi za robo fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya leo Jumatano
AC Milan v Napoli, saa 4:00 usiku
Real Madrid v Chelsea, saa 4:00 usiku
Kimataifa Haaland aweka rekodi mpya EPL
Haaland aweka rekodi mpya EPL
Read also