London, England
Chelsea inadaiwa kuanza mazungumzo na kocha wake wa zamani, Jose Mourinho ili arejee katika klabu hiyo na kurithi mikoba ya Graham Potter aliyetimuliwa.
Chelsea hivi karibuni ilimtimua Potter kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo na kumteua mchezaji wa zamani wa timu hiyo Frank Lampard kuwa kocha wa muda.
Vyovyote itakavyokuwa Lampard ambaye Januari mwaka huu alitimuliwa Everton, hatoweza kuendelea na timu hiyo baada ya msimu huu kumalizika hivyo ni wazi mabosi Chelsea wanasaka kocha mpya mwenye hadhi.
Aprili 12, Chelsea itakuwa na mtihani mzito wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid lakini mechi hiyo haijawatoa mabosi katika mbio za kusaka kocha mpya mwenye hadhi.
Mpango wa kumrudisha Mourinho Chelsea ukifanikiwa hiyo itakuwa mara yake ya tatu ndani ya klabu hiyo baada ya kuinoa kwa vipindi viwili tofauti na vyote ameondoka na mataji.
Mourinho au Special One ambaye kwa sasa anainoa AS Roma ya Italia pia zipo habari zisizo rasmi kuwa anatakiwa nchini Saudi Arabia kwa ofa ya Euro 120 milioni kwa mkataba wa miaka miwili.
Kocha mwingine ambaye amekuwa akihusishwa na Chelsea ni Luis Enrique ambaye inadaiwa kwamba hivi karibuni alikwenda London kwa ajili ya mazungumzo ya kuinoa timu hiyo.
Enrique, kocha wa zamani wa Barcelona na timu ya Taifa ya Hispania amekuwa hana kazi tangu ajiuzulu kuinoa Hispania baada ya matokeo mabaya kwenye fainali za Kombe la Dunia za Qatar Desemba mwaka jana.
Kimataifa Mourinho atajwa Chelsea
Mourinho atajwa Chelsea
Read also