Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars, Bakari Shime (pichani) ameita kikosi cha wachezaji 30 kitakachoingia kambini April 2, mwaka huu kujiandaa na mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Kenya.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo, mchezo huo ulipangwa kuchezwa Aprili 9, lakini huenda tarehe ikabadilika.
“Twiga Stars itacheza na Kenya na mchezo ulipangwa ufanyike April 9, mwaka huu, suala hili tutatolea ufafanuzi zaidi,” alisema Ndimbo kwa kifupi baada ya kutangaza kikosi hicho kwenye mitandao ya kijamii ya shirikisho hilo.
Wachezaji walioitwa ni Najat Abasi, Stumai Abdallah, Happy Hezron, Anastazia Katunzi, Donisia Minja, Jakline Shija na Eto Mlezi ambao wote wanatoka JKT Queens.
Wengine ni Fatuma Issa, Gelwa Yona, Amina Ramadhan, Ester Mayala wa Simba Queens), Amina Ally, Fumukazi Ally, Emiliana Mdimu, Lucia Mrema, Irene Kisisa, Janeth Christopher, Maimuna Kaimu, Zulfa Makau na Husna Mtunda (Yanga Princess).
Pia wamejumuishwa Protasia Mbunda na Ester Mabanza wa Fountain Gate na Anatoria Audax (The Tigers Queens), Julieth Singano (Juarez, Mexico), Opa Clement (Beskitas, Uturuki), Aisha Masaka (BK Hacken, Sweden), Fatuma Mwisendi (Nees Atromitou, Ugiriki), Zuwena Aziz (Nahaj, Morocco), Enekia Kasongo, Diana Lucas (Ausfaz, Morocco).
Kimataifa Shime aita 30 Twiga Stars
Shime aita 30 Twiga Stars
Read also