Na mwandishi wetu
Kocha mpya wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Adel Amrouche leo Ijumaa ameanza na mguu mzuri mechi yake ya kwanza na timu hiyo baada ya kuichapa Uganda Cranes bao 1-0.
Katika mechi hiyo ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2023) iliyopigwa nchini Misri, Stars ilinufaika na bao hilo pekee lililofungwa na Simon Msuva katika dakika ya 68.
Msuva nyota wa zamani wa Yanga ambaye kwa sasa anacheza soka nchini Saudi Arabia katika klabu ya Al-Qadsiah, alifunga bao hilo baada ya kuitumia vizuri pasi ya beki wa kulia wa Stars, Dickson Job.
Dakika tatu baada ya kuingia bao hilo, Cranes waliokuwa wenyeji wa mchezo huo walimtoa nahodha wao, Emmanuel Okwi ambaye pia amewahi kuzichezea timu za Yanga na Simba za Tanzania na kumuingiza Mato Kassim.
Stars nayo ilifanya mabadiliko ya mapema dakika ya 57 kwa kumtoa mshambuliaji Hamis Said Jr na nafasi yake kuchukuliwa na Abdul Seleman ‘Sopu’ mabadiliko ambayo yaliipatia Stars bao hilo pekee.
Mabadiliko mengine yaliyofanywa na Amrouche ni katika dakika ya 79 alipowatoa Mudathir Yahya na nafasi yake kuingia Feisal Salum au Fei Toto na zikiwa zimebaki dakika tano mpira kumalizika Msuva ambaye aliumia alitoka na nafasi yake kuingia Kelvin John.
Kwa ushindi huo Stars sasa inashika nafasi ya pili katika kundi lake ikiwa na pointi nne wakati Algeria ikiwa kinara wa kundi hilo Niger ni ya tatu na Uganda ambayo itarudiana na Stars Jumanne ijayo
jijini Dar es Salaam inaburuza mkia.
Kimataifa Amrouche aanza vizuri Stars
Amrouche aanza vizuri Stars
Read also
