Manchester, England
Kocha wa Man City, Pep Guardiola amesema mshambuliaji wake Erling Haaland anajitengenezea tatizo kutokana na ubora wa kiwango chake na kujikuta akitaka afunge mabao matatu (hat trick) kila mechi.
Haaland ameifungia Man City mabao manane katika siku tano, matatu katika ushindi wa 6-0 dhidi ya Burnley katika Kombe la FA na mengine matano dhidi ya RB Leipzig katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kwa msimu huu pekee hadi sasa Haaland amefunga jumla ya mabao 42 zikiwamo hat trick sita na Pep anasema kwamba ubora huo utamfanya awe na matarajio ya juu zaidi.
“Huyu mtu atakuwa na tatizo siku zijazo, watu wanatarajia kila mechi atafunga mabao matatu au manne na hilo halitowezekana kutokea,” alisema Pep.
“Watu wanatakiwa kusema machache, najua si mwenye kujali, anaangalia mbele na ana msimamo chanya katika maisha yake, si mwenye kulalamika anajiangalia yeye wakati wote, kwa vyovyote itakavyokuwa tukicheza vizuri tu ni lazima atafunga,” aliongeza Pep.
“Malengo aliyojiwekea ya kufunga sijui idadi yake lakini tukicheza katika ubora Erling ni lazima atafunga tu magoli,” aliongeza Pep.
Kimataifa Mabao ya Haaland yamshtua Pep
Mabao ya Haaland yamshtua Pep
Read also
