Na mwandishi wetu
Hatimaye kiungo mshambuliaji, Hassan Dilunga ameanza mazoezi rasmi na klabu ya Simba akitarajia kuiwakilisha klabu hiyo msimu ujao.
Dilunga amekuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya mwaka sasa akiuguza majeraha ya goti aliyoripotiwa kuyapata mwezi Februari mwaka jana wakati Simba ikijiandaa na mechi za hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Mchezaji huyo ambaye hakujumuishwa kwenye usajili wa Simba msimu huu baada ya kumalizika kwa mkataba wake msimu uliopita, ameanza mazoezi hayo jana kwenye Uwanja wa Mo Arena, Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kurejea mazoezini, Dilunga alisema: “Kifupi niseme nashukuru Mungu nimekaa nje muda wa mwaka sasa, majeraha ndio yameniweka nje na sasa nina afadhali kubwa ndani yangu ndio maana nimeanza mazoezi.”
Hata hivyo, taarifa zinafafanua kuwa Dilunga aliyewahi kukipiga Yanga, Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting yumo kwenye mipango ya Wekundu hao, akitarajiwa kupewa mkataba kuelekea msimu ujao.
Soka Dilunga aanza kujifua Simba
Dilunga aanza kujifua Simba
Read also
