Paris, Ufaransa
Klabu ya Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa inadaiwa kuwa mbioni kumrudisha kocha wake wa zamani, Thomas Tuchel ili kurithi mikoba ya Christophe Galtier.
Kocha huyo Mjerumani aliwahi kuinoa PSG kuaniza mwaka 2018 na kutimuliwa Desemba 2020 kabla ya kutua Chelsea na kujipatia mafanikio ikiwamo kuiwezesha timu hiyo kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Tuchel hata hivyo msimu huu haukuwa mzuri kwake baada ya Chelsea kujikuta katika wakati mgumu kweli Ligi Kuu England ikipoteza mechi hali iliyowafanya mabosi wa klabu hiyo kumtimua na nafasi yake kukabidhiwa Graham Potter ambaye naye kwa sasa ana wakati mgumu.
Kocha wa sasa wa PSG, Galtier katika siku za karibuni amekuwa akipitia kipindi kigumu baada ya kupata matokeo yasiyoridhisha hali ambayo imesababisha nafasi yake kuanza kujadiliwa.
Wakati huo huo mshambuliaji wa PSG, Neymar ambaye amekuwa akihusishwa na mipango ya kuihama timu hiyo amesema kwamba hana mpango wa kuhama kabla ya mkataba wake wa sasa kufikia ukomo mwaka 2027.
Neymar ambaye ni majeruhi, katika siku za hivi karibuni imekuwa ikielezwa kwamba mabosi wake wamekutana na mabosi wa Chelsea ili kuangalia uwezekano wa kuuziana mchezaji huyo.
Kimataifa PSG yataka kumrudisha Tuchel
PSG yataka kumrudisha Tuchel
Read also
