Manchester, England
Man United na Man City leo zinaumana katika mechi ya Ligi Kuu England huku beki wa zamani wa Man United, Patrice Evra akiipa ushindi timu yake ya zamani katika mechi hiyo.
Evra alisema kwamba hajawahi hata siku moja kuidharau Man City lakini anaamini Man United inaweza kuwaumiza Man City katika mechi hiyo maarufu Manchester Derby.
“United inaweza kuwaumiza Man City, sitowahi kamwe kuidharau City,” alisema Evra ambaye pia ni beki wa zamani wa timu ya Taifa ya Ufaransa ingawa pia alionekana kama kujichanganya hapo hapo kwa kusema kwamba ni mechi ya 50/50.
“City ni timu imara hasa na ni mtihani mkubwa kwa United, ni mechi ngumu kutabiri, Mahrez yuko vizuri na City yake kwa wakati huu, ni Derby kwa hiyo sitegemei kufungwa mabao mengi, ninachokiona ni United kushinda 2-1 lakini pia haitokuwa ajabu kwa City kushinda.”
Katika mechi hiyo itakayopigwa kwenye dimba la Old Trafford, United itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kutoishinda City katika uwanja huo tangu Machi 2020 na hivyo leo itataka kupindua matokeo.
Kwa upande mwingine United leo pia itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu nzuri kwenye dimba la Old Trafford, haijapoteza mechi katika uwanja huo tangu Septemba 8 mwaka jana ilipofungwa na Real Sociedad bao 1-0 katika mechi ya Europa Ligi na leo bila shaka itataka kuendeleza wimbi hilo la ushindi.
Kimataifa Evra aipa ushindi Man Utd kwa City
Evra aipa ushindi Man Utd kwa City
Related posts
Read also