London, England
Mshambuliaji mpya wa Chelsea, Joao Felix ameanza na mguu mbaya mechi yake ya kwanza akiwa na jezi ya Chelsea baada ya timu yake kufungwa mabao 2-1 na Fulham na yeye kupewa kadi nyekundu.
Felix alijiunga na Chelsea kwa mkopo juzi Jumatano akitokea Atletico Madrid kwa ada ya Pauni 9.7 milioni na mechi ya jana ilikuwa ya kwanza kwa nyota huyo wa Ureno kwenye Ligi Kuu England.
Mchezaji huyo sasa atakuwa anauguza matokeo mabaya ya timu yake mpya na kadi nyekundu aliyoipata kwa kumchezea rafu beki Kenny Tete katika dakika ya 58 inayomfanya akose mechi tatu.
Kabla ya kadi nyekundu, Felix ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Ureno alionyesha uwezo na mashabiki wa Chelsea kujiaminisha kwamba timu yao haikukosea kumsajili lakini kadi ilimkwamisha
Chelsea ilizamishwa kwa bao la dakika ya 72 lililofungwa kwa kichwa na Carlos Vinicius, hiyo ni baada ya Willian kuwapatia wenye Fulham bao la kwanza na Chelsea kusawazisha mapema kipindi cha pili kupitia kwa Kalidou Koulibaly.
Mtu mwingine anayeumizwa zaidi na matokeo mabaya ya Chelsea, ni kocha Graham Potter ambaye mambo yake yanazidi kuwa mabaya kutokana na mwenendo usioridhisha wa timu hiyo.
Kimataifa Joao aanza vibaya Chelsea
Joao aanza vibaya Chelsea
Read also
