Paris, Ufaransa
Lionel Messi jana Jumatano alicheza mechi yake ya kwanza ya Ligi 1 tangu kumalizika fainali za Kombe la Dunia kwa kuifungia bao Paris St-Germain (PSG) iliyotoka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Angers.
Nahodha huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 35 alikuwa na mapumziko marefu baada ya kuisaidia Argentina kubeba Kombe la Dunia Desemba 18 mwaka jana na tayari imeelezwa kwamba bado ana nafasi ya kuichezea Ufaransa katika fainali za Kombe la Dunia za 2026.
Kauli hiyo imetolewa na Kocha wa Argentina, Lionel Scaloni, “nafikiri Messi anaweza kucheza fainali zijazo za Kombe la Dunia, ingawa hiyo itategemeana na kile anachokitaka ambacho ataona kuwa ni kizuri kwake.”
Messi mwenyewe amewahi kunukuliwa akisema kwamba ataendelea kuichezea Argentina katika miaka michache ijayo baada ya kuiwezesha kubeba taji la dunia.
Katika mechi ya jana, Messi aliifungia PSG bao la pili dakika ya 72 baada ya Hugo Etike kufunga bao la kwanza dakika ya tano.
PSG kwa sasa inashika usukani wa Ligi 1 ikiwa na pointi 47 ikifuatiwa na Lens yenye pointi 41 ambayo ilitoka sare ya mabao 2-2 katika mechi yake na Strasbourg.
Katika mechi za Ligi 1 zilizochezwa jana matokeo ni kama ifuatavyo…
PSG 2-0 Angers
Ajaccio 0-1 Reims
Auxerre 0-5 Toulouse
Brest 0-0 Lille
Clermont 2-1 Rennes
Nantes 0-0 Lyon
Lorient 2-2 Monaco
Nice 6-1 Montpellier
Strasbourg 2-2 Lens
Troyes 0-2 Marseille
Kimataifa Messi aanza na bao PSG
Messi aanza na bao PSG
Related posts
Read also