Madrid, Hispania
Hatimaye klabu ya Atletico Madrid ya Hispania imetangaza dau kwa klabu inayomtaka nyota wake Joao Felix ambaye pia inadaiwa kwamba hana mahusiano mazuri na kocha, Diego Simeone.
Kwa Man United ambayo imekuwa ikidaiwa kumtaka mchezaji huyo sasa itatakiwa kutoa Pauni 9.5 milioni ikiwa ni kwa mkopo na kama inataka kumbeba jumla itatakiwa kulipa Pauni 70 milioni.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ambaye akiwa na timu ya Taifa ya Ureno kwenye fainali za Kombe la Dunia alianza kuhusishwa na mipango ya kuwania na klabu kadhaa barani Ulaya ingawa kwa wakati huo Atletico haikutaka kuzungumza lolote kuhusu nyota huyo wa nchini Ureno.
Habari za ndani hata hivyo zinadai kwamba kutokana na hali ngumu ya kifedha inayoikabili klabu hiyo suala la kumuuza mchezaji huyo ni jambo linalosubiri muda tu hasa kwa kuwa pia hana maelewano mazuri na kocha Simeone.
Simeone aliwahi kuzungumzia maelewano yake na mchezaji huyo na ingawa alikiri kwamba kulikuwa na tatizo lakini alifafanua kwamba ni jambo la kawaida kwamba kuna wakati wamekuwa wakipishana katika baadhi ya mambo.
Kimataifa Atletico yamtangazia dau Joao Felix
Atletico yamtangazia dau Joao Felix
Related posts
Read also