Saudi Arabia
Hatimaye winga, Cristiano Ronaldo amejiunga na klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia baada ya kuachana na Man United katika mazingira yaliyojaa utata.
Klabu ya Al Nassr imethibitisha Ijumaa jioni kwamba Ronaldo mwenye miaka 37 amesaini mkataba utakaomfanya aichezee timu hiyo hadi mwaka 2025 na inadaiwa kwa mwaka atakuwa akilipwa Dola 75 milioni na kumfanya awe mwanamichezo anayelipwa fedha nyingi.
“Nina furaha kubwa kuingia kwenye ligi mpya ya soka katika nchi tofauti kabisa,” alisema Ronaldo katika taarifa iliyotolewa na Al-Nassr.
“Kile wanachokifanya Al Nassr katika kuiendeleza Saudi Arabia kwenye soka la wanawake na wanaume ni mambo yanayovutia, tumeweza kuliona hilo kwa kiwango cha soka la Saudi Arabia kwenye fainali za Kombe la Dunia hivi karibuni, hii ni nchi yenye matamanio makubwa na ina fursa nyingi kwenye soka,” alisema Ronaldo.
“Nina bahati kwa kushinda kila nilichodhamiria kushinda katika soka la Ulaya, na naona huu ni wakati sahihi kutumia uzoefu wangu Asia, najiandaa kukutana na wachezaji wenzangu wapya na kwa pamoja tuisaidie Al Nassr kupata mafanikio,” aliongeza.
Ronaldo alilazimisha kuondoka katika klabu ya Man United siku chache kabla ya fainali za Kombe la Dunia kwa kuvunja mkataba baada ya kufanya mahojiano ambayo yaliwasema vibaya baadhi ya mabosi wa klabu hiyo akiwamo kocha Eric ten Hag.
Inadaiwa baada ya kuondoka Man United na Ureno kutolewa kwenye fainali za Kombe la Dunia, Ronaldo amekuwa akifanya mazoezi katika klabu ya Reala Madrid huku uvumi ukimhusisha kujiunga na klabu kadhaa ikiwamo Al Nassr ambayo hatimaye amejiunga nayo.
Kimataifa Ronaldo asaini Al-Nassr
Ronaldo asaini Al-Nassr
Related posts
Read also