Na mwandishi wetu
Winga wa Yanga, Denis Nkane atakuwa nje ya uwanja kwa wiki sita baada ya vipimo kuonesha kuwa amevunjika mfupa mdogo unaosababisha nyonga kujikunja. Daktari wa timu hiyo, Moses Etutu amethibitisha.
Akizungumza Dar es Salaam leo daktari huyo alisema Nkane atakuwa na vipindi viwili vya kuuguza majeraha yake yatakayochukua takriban wiki nne hadi hapo atakaporejea rasmi uwanjani.
“Vipimo vimeonesha alivunjika mfupa unaosababisha nyonga kukunja ndiyo maana alipata maumivu makali sana. Tayari tumeshaanza ratiba ya matibabu na atakuwa na vipindi viwili kabla ya kurejea moja kwa moja uwanjani,” ilisema daktari huyo katika taarifa yake.
Nkane aliumia katika mchezo dhidi ya Coastal Union na kukosekana katika michezo kadhaa iliyopita huku pia akitarajiwa kutoonekana kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi itakayoanza Januari Mosi, mwakani visiwani Zanzibar kutokana na tatizo la jeraha lenyewe.
Dk Etutu alisema kwamba katika wiki hizo nne atakazokuwa nje, wiki mbili za mwisho mchezaji huyo ataanza mazoezi mepesi ambayo atakuwa anamfuatilia kujua maendeleo yake kabla ya kurejea dimbani akiwa kamili.
Soka Nkane nje wiki sita
Nkane nje wiki sita
Related posts
Read also