Paris, Ufaransa
Kocha wa klabu ya Paris Saint-Germain (PSG), Christophe Galtier amekanusha madai ya kuwapo kwa ugomvi kati ya Lionel Messi na Kylian Mbappe baada ya wachezaji hao kushindana kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Dunia.
Messi aliibuka shujaa kwa kuiwezesha Argentina kubeba taji la dunia kwa ushindi wa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya dakika 120 ngumu zilizoisha kwa sare ya mabao 3-3.
Katika mechi hiyo, Messi ambaye ni nahodha wa Argentina alifunga mabao mawili wakati Mbappe alikuwa mchezaji wa pili katika historia ya fainali za Kombe la Dunia kwa wanaume kwa kufunga mabao matatu (hat trick).
Mbappe tayari amerejea katika kikosi cha PSG na huenda akacheza mechi ya leo Jumatano ugenini dhidi ya Strasbourg na Galtier amesema kwamba Mbappe ameumizwa mno kwa kutobeba taji la dunia lakini alimpongeza mchezaji huyo kwa hulka zake.
“Hakuna sababu ya kuchanganya kila kitu katika uhusiano kati ya Kylian na Leo (Messi), Kylian amekuwa mwenye hulka sahihi baada ya kulikosa taji la dunia,” alisema Galtier.
“Unapolikosa Kombe la Dunia unakuwa na kila sababu ya kukosa raha, kujiona mnyonge lakini anajua namna nzuri ya kuangalia yajayo na kuendelea kupambana na amekuwa muungwana kwa kumpongeza Leo (Messi) na hilo ni jambo zuri kwa klabu na timu,” aliongeza Galtier.
Glatier pia alisema kwamba Messi atarudi kwenye kikosi cha PSG mwanzoni mwa mwezi Januari na hivyo bingwa huyo mara saba wa Ballon d’Or ataikosa mechi dhidi ya Strasbourg na inayofuata ya ugenini dhidi ya Lens itakayopigwa Jumapili.
Kimataifa ‘Mbappe, Messi hawana ugomvi’
‘Mbappe, Messi hawana ugomvi’
Related posts
Read also