Na mwandishi wetu
Kinara wa mabao wa Ligi Kuu ya NBC msimu uliopita, George Mpole hatimaye amekamilisha rasmi shauku yake ya kutaka changamoto mpya baada ya kusaini mkataba wa kujiunga na klabu ya FC Saint-Eloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mpole ambaye baada ya kuaga rasmi katika klabu ya Geita Gold, habari zilianza kuvuma kwamba alikuwa mbioni kujiunga na moja ya vigogo vya soka nchini lakini baadaye zikaja habari nyingine ambazo hazikuthibitishwa kwamba alikuwa katika mazungumzo na klabu ya FC Lupopo.
Taarifa zinaeleza zaidi kuwa mshambuliaji huyo aliyeibuka mfungaji bora kwa kupachika mabao 17 akiwa na Geita Gold na kumpiku Fiston Mayele wa Yanga, amesaini mkataba wa miaka miwili na timu hiyo ikiwa ni wiki mbili zimepita tangu aachane na Geita.
Mpole kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram katika kipengele cha InstaStory ameweka picha akiwa ameshika bendera ya Lupopo na kuandika kuwa sasa yuko kwenye makazi yake mapya.
Tangu kuanza kwa msimu huu mchezaji huyo awali aliingia katika mgogoro na mabosi wa Geita kwa kilichoelezwa kuwa alikuwa akidai haki zake lakini baadaye aliibuka na kusema kwamba yeye na Geita hawadaiani na ameamua kwa hiari yake kuondoka katika klabu hiyo kwa lengo la kusaka changamoto mpya kwingineko.
Soka Mpole rasmi FC Lupopo
Mpole rasmi FC Lupopo
Related posts
Read also