Na mwandishi wetu
Timu ya Soka ya Wanawake, Yanga Princess imeamua kufanya maandalizi yake walipo kaka zao, Avic Town Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa derby dhidi ya Simba Queens utakaopigwa esemba 22, mwaka huu.
Mratibu wa kikosi hicho, Kibwana Matokeo alisema Avic Town inastahili kwao kulingana na mazingira mazuri yenye utulivu kwa kujiandaa na mechi ngumu kama hiyo.
Alisema kuwa wachezaji wakikutana na kaka zao itawajengea kujiamini na kujiandaa vizuri kwa pambano hilo ambalo wamedhamira kufanya vizuri ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa mwisho wa msimu.
“Tumefanya uamuzi huo kwa sababu kubwa mbili, kwanza kocha anahitaji mazingira mazuri ya kutengeneza muunganiko mzuri kwa timu zote mbili, wanaume na wanawake lakini pia itatusaidia kuwajengea uwezo mabinti wetu kujiamini sana,” alisema.
Kuhusu derby, Yanga imekutana na Simba mara 10 na kati ya hizo imeshinda mchezo mmoja ikionekana ni kibonde kwa Wekundu hao lakini safari hii huenda wakarudi kivingine wakiwa chini ya kocha wao mpya, Sebastian Nkoma aliyekuwa akiinoa Queens msimu uliopita.
Soka Princess waiendea Simba Avic Town
Princess waiendea Simba Avic Town
Related posts
Read also