Na mwandishi wetu
Kocha wa Yanga Princess, Edna Lema ameeleza kukosa uzoefu wa ligi kwa wachezaji wao wapya kulichangia kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Fountain Gate huku akiwapongeza wapinzani wao kwa ushindi huo.
Yanga Princess ilipoteza mechi hiyo iliyopigwa jana kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ikiwa ni mechi ya kwanza ya msimu huu kwa Ligi ya Wanawake.
Lema alifafanua kuwa hawakuzidiwa katika mchezo huo isipokuwa kulikosekana morali ya uzoefu kwa wachezaji wao wengi ambao ndiyo mara ya kwanza wanacheza Tanzania japokuwa baadaye walirejea mchezoni lakini haikuwa rahisi kupindua matokeo hayo.
“Nafikiri sio kuzidiwa, sababu mechi ilipoanza kuna wachezaji wetu wengi ndiyo kwanza walikuwa wanacheza ligi ya Tanzania walikuwa chini, mapumziko nilizungumza nao ndiyo maana waliporudi walicheza vizuri lakini mwisho tulipoteza.
“Nawapongeza Fountain kwa kupata matokeo, wameanza vizuri lakini ndiyo kwanza ligi imeanza naamini tuna nafasi nyingine ya kufanya vizuri zaidi maana ndiyo kwanza ligi imeanza,” alisema Lema.
Nye kocha wa Fountain, Alex Alumira alisema: “Kikubwa nawashukuru wachezaji wangu wamefuata maelekezo, wamekuwa na nidhamu ya ukabaji na ndiyo maana wamejizawadia ushindi kwa juhudi zao, ligi ndiyo kwanza imeanza na hakuna timu dhaifu bado tunahitaji kujipanga zaidi.”
Soka Uzoefu waiangusha Yanga Princess
Uzoefu waiangusha Yanga Princess
Related posts
Read also