Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa Geita Gold, George Mpole leo Jumatano ameachana rasmi na klabu hiyo baada ya makubaliano ya pande zote mbili waliyoafikiana hivi karibuni.
Taarifa ya Mpole kumalizana na timu hiyo imeibuka muda mfupi uliopita baada ya kuonekana kwa barua ya uongozi wa Geita inayomtakia kila la heri mchezaji huyo ambaye hivi karibuni waliingia nayekwenye mtafaruku.
Barua hiyo inayoonesha imesainiwa na Mtendaji Msaidizi, Ramadhan Bukambu imeeleza kuwa inamshukuru Mpole kwa huduma yake kwa muda wote aliokuwa Geita mpaka wanakubaliana kusitisha mkataba, hivyo wanamtakia kila heri aendako.
Hata hivyo, kabla ya taarifa hiyo, Mpole alikuwa kwenye mgogoro na uongozi wa Geita na kutoweka katika timu hiyo kwa zaidi ya wiki nne kabla ya kurejea hivi karibuni ikielezwa yupo kwenye mazungumzo na uongozi kabla ya leo kuibuka habari hiyo mpya.
Mpole amekuwa akihusishwa kuwaniwa na timu za Simba na Yanga tangu alipokuwa mfungaji bora msimu uliopita wa Ligi Kuu ya NBC akipachika mabao 17 ambapo sasa inadaiwa kwamba inaweza kuwa nafasi nzuri ya kuangalia maisha mapya ndani ya kikosi kingine.
Soka Mpole, Geita Gold waachana
Mpole, Geita Gold waachana
Related posts
Read also