Na mwandishi wetu
Uongozi wa timu ya Ruvu Shooting leo Jumanne, umemtangaza Mbwana Makata kuwa kocha mpya wa timu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja akichukua mikoba iliyoachwa na Charles Mkwasa aliyeachia ngazi hivi karibuni.
Ofisa Habari wa Ruvu, Masau Bwire ameeleza kuwa wamemchagua Makata kwa sababu wanajua uwezo wake na wana imani atabadili mwenendo wa timu yao.
“Tunamshukuru Mkwasa kwa kazi nzuri na tunamtakia maisha mema huko anakokwenda katika maisha yake ya mpira lakini pia tunamkaribisha Makata na imani yetu atatupa mafanikio katika kipindi cha mwaka huo mmoja atakaokuwa na sisi,” amesema Bwire.
Bwire amefafanua kuwa malengo yao ni kuhakikisha Ruvu Shooting inafanya vizuri hivyo wamepanga kufanya usajili mzuri zaidi kwenye dirisha dogo ili warejee kwenye ushindani.
Ruvu kwa sasa inashika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC ikiwa na pointi 11 katika michezo 15 iliyocheza kwenye mzunguko wa kwanza, ikiwa imeshinda mechi tatu, sare mbili na ikifungwa mechi 10.
Makata amepewa mikoba hiyo ikiwa ni wiki chache tangu amalize adhabu yake ya kufungiwa miezi sita kutokana na kuwashawishi wachezaji wasiingie uwanjani kucheza mechi dhidi ya Namungo akidai utaratibu wa usalama wa wachezaji umekiukwa.
LigiKuu Makata amrithi Mkwasa Ruvu
Makata amrithi Mkwasa Ruvu
Related posts
Read also