Na mwandishi wetu
Kocha wa Simba, Juma Mgunda amewataka wachezaji wake wasikate tamaa katika vita ya kuishusha Yanga kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mgunda ameeleza hayo kutokana na pengo la pointi lililopo kati ya timu hizo mbili ambapo Yanga inaongoza ikiwa na pointi 32 baada ya mechi 13 dhidi ya watani zao Simba waliopo nafasi ya tatu na pointi 31 katika mechi 14.
Yanga jana Jumanne ilishuka dimbani dhidi ya Ihefu FC na kulala kwa mabao 2-1 na hivyo kushindwa kuongeza gepu la pointi kati ya timu hizo mbili zenye maskani yake Dar es Salaam na kibaya zaidi matokeo hayo yalifuta rekodi ya timu hiyo kutopoteza mchezo tangu kuanza kwa ligi.
Kocha huyo ameeleza kuwa anatambua vita ya kuwaondoa Yanga kwenye nafasi ya kwanza siyo ndogo lakini hawapaswi kukata tamaa zaidi ya kuendeleza mapambano kwa kushinda mechi zao.
“Hii ni vita kubwa lakini kwa ukubwa wetu Simba hatupaswi kukata tamaa tunatakiwa kuongeza kasi ya mapambano na kuhakikisha tunashinda kila mechi iliyopo mbele yetu na mwisho wa msimu tutajua tupo nafasi gani,” alisema Mgunda.
Kocha huyo alisema kitu cha msingi anachokifanya kama kocha ni kuhakikisha viwango vya wachezaji wake pamoja na kupandisha ari na hamasa ya upambanaji kwa wachezaji hao akiamini hiyo itawasaidia katika kutimiza malengo yao.
Alisema anajua ligi ni ngumu na timu nyingi zimejiandaa vizuri lakini kwa ukubwa waliokuwa lazima wahakikishe malengo yao ya kuiondoa Yanga kileleni yanatimia na kuongoza ligi ili pia kurejesha heshima yao ndani ya ligi.
Kati ya mechi 14 walizocheza Simba msimu huu wamefungwa mechi moja, sare mechi nne na wameshinda mechi tisa wakati watani zao Yanga katika mechi 12 walizocheza msimu huu wameshinda mechi 10, wameshindwa mechi moja na kwenda sare mechi mbili.
Soka Mgunda: Hakuna kukata tamaa
Mgunda: Hakuna kukata tamaa
Related posts
Read also