Doha, Qatar
Baada ya Japan kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ujerumani, mashabiki wake waliahirisha sherehe za ushindi, wakaamua kujitolea kuokota uchafu kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Khalifa.
Kwenye viwanja vya soka, mechi inapomalizika kunakuwa na uchafu wa kila aina, kuanzia chupa za maji na vinywaji vingine, mabaki ya vyakula mbalimbali na vifungashio vyake, kwa mashabiki wa Japan hali hiyo waliamua kuitumia kutoa somo la kujali mazingira na usafi.
Kutoka na ushindi mbele ya Ujerumani, Taifa kubwa kwenye soka duniani, halikuwa jambo dogo, ilihitaji kulifurahia mara baada ya filimbi ya kumaliza mchezo kupulizwa, lakini mashabiki wa Japan wakajisahaulisha na kuukumbusha uma wa wanamichezo kwamba usafi na utunzaji mazingira ni jambo lenye maana kubwa pengine kuliko ushindi dhidi ya Ujerumani.
Kwa watu wa Japan suala la usafi ni kama utamaduni ambao mtoto anafundishwa tangu akiwa mdogo na ndio maana haishangazi kuona mashabiki wa soka wa nchi hiyo, maarufu Samurai Blue wakijitoa kimasomaso bila malipo kuokota uchafu.
Tukio hilo la Qatar si la kwanza kwa mashabiki hao, miaka mianne iliyopita walifanya hivyo nchini Urusi mara baada ya mechi yao na Ubelgiji, mechi ambayo walifungwa mabao 3-2 lakini baada tu ya matokeo hayo mabaya, mashabiki hao wakaanza wakaanza kuokota uchafu wakiwa na huzuni lakini majuzi wameifanya kazi hiyo wakiwa na furaha kuonyesha kwamba usafi ni utamaduni wao.
Mashabiki hao pia waliifanya kazi hiyo ya kuokota uchafu katika mechi ya ufunguzi kati ya wenyeji Qatar na Ecuador na hivyo kudhihirisha kwamba wanachokifanya wamekidhamiria.
Japan ambayo ipo Kundi E, itacheza mechi yake ya pili Jumapili dhidi ya Costa Rica kabla ya kumalizia mechi za makundi dhidi ya Hispania Alhamisi ijayo.
GreenSports Mashabiki Japan wazoa takataka uwanjani
Mashabiki Japan wazoa takataka uwanjani
Related posts
Read also