Manchester, England
Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola ameongeza miaka miwili katika mkataba wake na klabu hiyo na hivyo ataendelea kukinoa kikosi hicho hadi mwaka 2025.
Pep kocha wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich, hadi sasa ameiwezesha timu hiyo kutwaa mataji 11 yakiwamo manne ya Ligi Kuu England katika kipindi cha miaka sita tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Bayern.
“Tangu siku ya kwanza niliona kuwa hapa ni kitu cha kipekeee, nina furaha kuendelea kubaki Manchester City kwa miaka mingine miwili,” alisema kocha huyo kutoka Hispania aliyejipatia mafanikio zaidi akiwa na Barca.
“Siwezi kutoa shukrani za kumtosha kila mtu katika klabu hii kwa jinsi walivyoniamini, nina furaha na nimeridhika na nina kila kitu ninachohitaji cha kufanya kazi yangu katika namna bora kadri iwezekanavyo,” aliongeza Pep.
“Najua ukurasa unaofuata wa klabu hii utakuwa wa aina yake kwa miaka 10 ijayo, ilitokea hivyo kwa miaka zaidi ya 10 iliyopita na itatokea tena katika miaka 10 ijayo, kwa sababu klabu iko imara sana, bado nina fikra kwamba kuna mambo mengi zaidi tunayoweza kuyafanikisha pamoja na ndio maana nataka kubaki na kuendelea kupigania mataji,” alisema.
Man City ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England kwa sasa wanashika nafasi ya pili nyuma ya vinara Arsenal kwa tofauti ya pointi tano lakini pia wamefuzu hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na sasa wanasubiri kuumana na RB Leipzig, Februari mwakani.
Kimataifa Pep asaini miaka 2 Man City
Pep asaini miaka 2 Man City
Related posts
Read also