Na mwandishi wetu
Kiungo wa klabu yaYanga, Khalid Aucho ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka kutoka nchini Uganda na kuwashukuru wote waliofanikisha ushindi wake huo.
Aucho, ametwaa tuzo hiyo jana ambayo ilichukuliwa na Thadeo Lwanga msimu uliopita alipokuwa akikipiga Simba SC kwa kuwapiku kipa wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Denis Onyango (37) na mshambuliaji wa Vipers, Yunus Sentamu.
Hii ni mara ya pili Sentamu anarejea kwenye kinyang’anyiro hicho na kuanguka baada ya msimu uliopita kutua kwa Lwanga ambaye kwa sasa anakipiga Arta Solar 7 ya Djibouti.
Aucho ambaye makabrasha yake yanaonesha ana miaka 29, amekuwa kwenye kiwango kikubwa tangu alipotua Yanga msimu uliopita akitokea Masr El Makasa ya Misri na kuisaidia timu hiyo kutwaa mataji ya Ligi Kuu, Kombe la FA na Ngao ya Jamii.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Aucho anayemudu nafasi za kiungo wa kati na mkabaji amewashukuru wote waliompigia kura katika tuzo hiyo, akisisitiza anaheshimu mchango wao na Mungu awabariki sana.
Soka Aucho atwaa tuzo Uganda
Aucho atwaa tuzo Uganda
Related posts
Read also