Buenos Aires, Argentina
Mashabiki waliojihusisha na matukio haramu ya uhalifu ni kati ya raia 6,000 wa Argentina ambao hawataruhusiwa kuingia kwenye viwanja vya soka kushuhudia mechi za fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Qatar kuanzia Novemba 20 mwaka huu.
Waziri wa Sheria na Usalama wa Argentina, Marcelo D’Aleesandro ilisema, “wafanya vurugu wapo hapa na pia wapo Qatar, tunataka kurudisha amani kwenye soka, wanaofanya vurugu lazima wawe nje ya viwanja vya soka. Watu hawa wamo kwenye makundi ya mashabiki wahalifu, wanaoshiriki katika vitendo vya vurugu, ulevi na wenye madeni,” aliongeza D’Alessandro.
Katika kuhakikisha usimamizi wa suala hilo unafanyika kama ilivyo kwenye fainali nyingine za Kombe la Dunia, ujumbe wa Argentina ukiwa na makundi tofauti tofauti ya wana usalama wataenda kufanya kazi ya kudhibiti wahalifu hao kwa kushirikiana na maofisa usalama wa Qatar.
Mwezi Juni mwaka huu, wizara ya usalama wa taifa nchini Argentina ilisaini mkataba wa ushirikiano na ubalozi wa Qatar wenye lengo la kuwadhibiti mashabiki wa Argentina wanaofahamika kwa vitendo vya vurugu na uhalifu viwanjani kutoruhusiwa kwenda kushuhudia mechi za Kombe la Dunia.
Miongoni mwa mshabiki 6,000 wa Argengtina waliopigwa marufuku kuonekana kwenye viwanja vya soka vya Qatar wakati wa fainali za Kombe la Dunia, wamo mashabiki 3,000 ambao tayari wamepigwa marufuku kushuhudia mechi za ligi za soka za Argentina.
Kimataifa Mashabiki 6,000 Argentina marufuku Qatar
Mashabiki 6,000 Argentina marufuku Qatar
Related posts
Read also