Na mwandishi wetu
Kocha wa Azam FC, Kali Ongala amesema licha ya timu yake kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu jana, amesema bado safari yao ya kusaka mafanikio ni ndefu na wanapaswa kuendelea kujifunza na kupambana.
Matokeo ya mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, umeipandisha Azam yenye maskani yake Chamazi hadi nafasi ya tatu kwa kufikisha pointi 17.
Ongala anayekaimu nafasi ya kocha mkuu ya timu hiyo tangu kutimuliwa kwa Denis Lavagne hivi karibuni alisema wana safari ndefu ya kuhakikisha wanaendelea kufanya vizuri katika michezo yao kulingana na ubora wa ligi yenyewe.
“Tunashukuru tumepata pointi tatu, tumejifunza mechi hii na bado tunaendelea kujifunza kwamba kuna muda mechi inaweza kuwa nzuri usipate matokeo na muda mwingine mechi ikawa ngumu na ukapata pointi tatu, tunahitaji kupambana zaidi,” alisema.
Ongala alisema wanahitaji kuimarika kidogo kidogo kutoka mechi moja kwenda nyingine na kuwatia moyo wachezaji kwa kuwaaminisha ili wacheze vizuri kwa kujituma.
“Bado barabara ndefu kuna njia nyingi inabidi tuimarike, tutawaaminisha wachezaji wacheze. Sisi benchi la ufundi tunajifunza na wachezaji wanaendelea kujifunza, naamini kwa kikosi kizuri tutafikia malengo yetu,” alisema.
Azam FC inapata ushindi wa pili mfululizo baada ya kutoka kuifunga Simba katika mchezo wa mzunguko wa nane ushindi sawa na huo, imewasha taa ya kijani.
Soka ‘Azam safari bado ndefu’
‘Azam safari bado ndefu’
Related posts
Read also