London, England
Kiungo wa klabu ya Brighton, Enock Mwepu amelazimika kustaafu soka akiwa na miaka 24 kutokana na matatizo ya moyo yaliyomkuta.
Taarifa ya klabu ya Brighton ilieleza kuwa, Mwepu anaweza kuwa katika hali ya hatari kama akiendelea Mwepu aliugua na kuwa dhaifu wakati akiwa na timu ya Taifa ya Zambia iliyokuwa safari ni nchini Mali mwezi uliopita kiasi cha kushindwa kufanya mazoezi na kulazwa hospitali kwa siku nne.
Baadaye Mwepu alirudi England na kujiunga na klabu yake ya Brighton lakini baada ya kufanyiwa vipimo matokeo yalionyesha kwamba suluhisho pekee kwa mchezaji huyo ni kustaagfu soka uamuzi.
“Vipimo vimeonyesha kuwa maradhi yake ni kama ya kurithi ambayo kwa siku za baadaye yanaweza kuongezeka zaidi na kuwa makubwa na ambayo awali vipimo havikuonyesha kuwapo kwa tatizo lolote,” ilieleza taarifa ya Brighton.
“Inasikitisha kwamba tatizo hili linaweza kujidhihirisha kupitia uchezaji wake wa soka, kwa hiyo Enock ameshauriwa kwamba suluhisho pekee kwa ajili ya usalama wake ni kwa yeye kuacha kucheza soka.
Akizungumzia uamuzi huo, Mwepu alisema kwamba jambo hilo limemsikitisha sana kwa sababu tayari alishafikia ndoto yake ya kucheza soka kwenye Ligi Kuu England lakini sasa baadhi ya ndoto zake zinalazimika kukatishwa.
“Hata hivyo hii haiwezi kuwa sababu ya mimi kuacha kabisa kujihusisha na soka, najipanga ili kuendelea kujihusisha na soka katika majukumu mengine,” alisema Mwepu kupitia akaunti yake ya Twitter.
Mwepu alijiunga na Brighton Julai, 2021 akitokea Red Bull Salzburg na kusaini mkataba wa miaka minne kwa ada ya Pauni 18 milioni, ameifungia timu hiyo mabao matatu katika mechi 27 na mara ya mwisho aliichezea timu hiyo Septemba dhidi ya Leicester ilipoibuka na ushindi wa mabao 5-2.
Mkuu wa kitengo cha tiba wa klabu ya Brighton, Adam Bret alisema, ” ni pigo kubwa kwa Enock lakini ni lazima aiweke mbele afya yake na familia yake na hivyo huu ni uamuzi sahihi licha ya kwamba analazimika kuachana na mchezo aupendao.
Mmoja wa wachezaji anayekumbukwa kwa kukumbwa na tatizo la moyo ni Fabrice Muamba ambaye alianguka uwanjani kutokana na matatizo ya moyo mwaka 2012 na kulazimika kustaafu soka lakini mwaka 2003 kiungo wa Cameroon Marc-Vivien Foe alifariki baada ya kuanguka uwanjani nchini Ufaransa wakati akiiwakilisha timu yake ya Taifa.
Kimataifa Mwepu astaafu soka akiwa na miaka 24
Mwepu astaafu soka akiwa na miaka 24
Related posts
Read also
